matangazo

matangazo

Friday, August 12, 2011

MH

Wadau nisaidieni eti huyu ni nani?

Wednesday, December 29, 2010

Wanahabari

Wanahabari wakiwa katika picha ya pamoja.Kutoka kushoto ni Geofrey Sima, katikati ni Tulizo Kilaga (afisa habari wizara ya maliasili na utalii) na mzalendo Lukelo Mshaura (afisa uhusiano Halmashauri ya Wilaya Njombe) wote hawa wamesoma chuo kikuu kishiriki cha Tumaini Iringa. Hapa tukiwa Mbeya kushiriki kikao kazi cha maafisa habari, elimu na mawasiliano wa Idara, Taasisi na Wakala wa serikali.Kikao hicho kilifanyika kuanzia tarehe 17 hadi 22 jijini Mbeya.

Wednesday, October 6, 2010

ZAMA ZA KALE


Mzalendo Lukelo ukijaribu kupekesha vijiti kama walivyofanya mababu zetu hapo zamani ili kuweza kupata moto. Licha ya zoezi hilo kuwa ni gumu lakini mungu si Athumani alifanikiwa kuupata moto.Chini ya vinavyopekechwa kuna kinyesi cha ng'ombe ambacho husaidia kudaka moto pindi vijiti vinapotoa cheche baada ya kupekechwa . Hapa ilikua mkoani Iringa katika kijiji cha Ilolo mpya kilichopo tarafa ya Pawaga kwenye maadhimisho ya wiki ya utalii.

Friday, August 6, 2010

vuvuzela la bongo

Mkimbiza mwenge kitaifa ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Masai kutoka mkoa wa Manyara akipuliza pembe la ng'ombe ambalo sauti yake vuvuzela la Afrika Kusini halioni ndani. Kuna uwezekano mkubwa kuwa vuvuzela asili yake ni vifaa kama hivi vya asili kwani hata Wanyasa, Wangoni,Wapangwa wanavifaa vyao vya asili ambavyo wanavitumia katika kunogesha na kuchangamsha shughuri mbalimbali na hutoa sauti mithili ya vuvuzela.

KIBURUDANI ZAIDI


Wanafunzi wa shule ya sekondari Wanike wakifurahia kuona mwenge ulipofika shule kwao ambako ulizindua jengo la utawala wa shule hiyo jengo ambalo ni la kisasa.Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Bw. Nassoro Ally Matuzya aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii kwani wanajengo zuri na lakisasa.

KIPAJI POPOTE TU



Wakimbiza mwenge kitaifa wakionyesha umahiri wao wa kucheza na kughani wakati mwenge ulipofika shule ya sekondari Wanike na kufungua jengo la utawala la shule hiyo iliyopo wilayani Njombe mkoani Iringa.

JIWE LA MSINGI


SARE YA NJOMBE


Hii ni sare iliyotumiwa na wilaya ya Njombe wakati wa kuukimbiza mwenge wilayani humo.

SARE

Hii ni sare ya mwenge iliyotumiwa na wilaya ya Ludewa.

KARIBU MWANANGU

Mkuu wa wilaya yaNjombe Bi Sara Dumba akimkumbatia mmoja wa viongozi wa mbio za mwenge wilipowasili wilayani Njombe

Thursday, August 5, 2010

KAMA UTANI VILE





Picha juu alianza kama utani vile kwa mwendo wa ukakamavu . Baada ya mwendo wa kikakamavu akafanya manjonjo kwa kufagilia kibunge mheshimiwa spikaaaaaaaaaaaaaa.huyo ni mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa ambaye anajulikana kwa jina la utani Masai kutoka Manyara akiwafurahisha wananchi kwa kufagilia kibunge.Hongera kwa ubunifu.

USIONE UKADHANI


Ngoma hiyo hapo juu ikipigwa matokeo yake unayapata kama inavyoonekana katika picha ya hapo chini baadhi ya viongozi wa serikali wakiserebuka kusubilia mwenge

raha ya ngoma


Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi Sara Dumba akiserebuka ngoma iliyokuwa ikipigwa na wanafunzi wakati wa kusubili mwenge wilayani Njombe

NGOMA INOGILE




Hivi ni baadhi ya vikundi vya Ngoma za asili wilaya ya Ludewa na Njombe vikitoa burudani kwenye mbio za mwenge mpakani mwa Ludewa na Njombe.Ngoma hii ikipigwa we acha tu kwani unajikuta unaingia uwanjani bila kupenda.Utamu wa ngoma...........

USALAMA KWANZA



Picha ya chini mzalendo Lukelo akiwa na mmoja wa walinda amani siku ya mwenge wilayani Njombe.Picha ya kwanza kushoto ni kamanda wa polisi Iringa na kushoto ni OCD wa wilaya yaNjombe kamanda E. Urio wakihakikisha usalama unakuwepo wakati wa makabidhiano ya mwenge mpakani mwa Njombe na Ludewa kijiji cha Kitulila mwenge ulipokabidhiwa kutoka wilaya ya Ludewa kuja Njombe.Katika ni mgambo shupavu akionyesha ukakamavu.

MWENGE UKIWASILI



Mwenge wa uhuru ukiwa mpakani mwa Njombe na Ludewa kabla ya kuanza kukimbizwa wilayani Njombe. hao ni baadhi ya wakimbiza mwenge kitaifa waliongozwa na Nassoro Ally Matuzya.Kazi zilizofanywa na mwenge wa uhuru mwaka 2010 wilayani Njombe ni kuweka jiwe la msingi ukumbi wa shule ya msingi Senga, Kukagua hifadhi ya msitu Isalilo,Kufungua zahanati Nundu na kukagua miche ya chai,kukagua ofisi za idara ya maji halmashauri ya Mji Njombe. mbali na hayo pia kufungua tanki la maji na barabara ya chai(Itombololo), kufungua jengo la utawala shule ya sekondari Wanike, kukagua chuo cha ufundi Igwachanya RC na kufungua soka la Igwachanya na baadae mwenge ulikabidhiwa kijiji cha Ludodolelo kilicho mpakani mwa Njombe na Makete tayari kwa kukimbizwa wilaya ya Makete.

SIO TIMU YA MPIRA




Wanaonekana kama ni kama wanamichezo fulani hivi ,lakini ukweli hao ni viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Njombe na halmashauri ya mji waNjombe wakiusubili mwenge mpakani mwa Ludewa na Njombe tayari kuukimbiza wilaya ya Njombe. Hii ni sare ya wilaya ya Njombe katika kuupokea mwenge wa uhuru mwaka huu 2010.

MWENGE UKIWASILI NJOMBE



Gari lililobeba mwenge likiwasili katika kijiji cha Kitulila kijiji ambacho kiko mpakani mwa wilaya ya Njombe na Ludewa.Mwenge ulikuwa ukitokea wilaya ya Ludewa

MAMBO YA MWENGE NJOMBE 31.07.2010


vuvuzela jipya

hii ni moja ya aina ya ushangiliaji iliyotumika kuukaribisha mwenge wilayani njombe. nilivutiwa sana na ubunifu huu kumbe hata hapa bongo vuvuzela zipo. wadau mnasemaje kuhusu vuvuzela hili ambalo ni bomba la chuma linalotumika katika mashine na lina sauti kubwa balaa

Monday, December 14, 2009

MANZARI

siku chuo cha Tumaini kilipowatunuku wazalendo wa fani mbalimbali hali ilikuwa hivi kwenye jukwaa. BAADA YA KUPATA BARUA PEPE NYINGI MZALENDO LUKELO ATAWALETEA MATUKIO MBALIMBALI YA MAHAFALI YA CHUO CHA TUMAINI IRINGA

HONGERA

Siku mzalendo Lukelo(wakwanza kulia) alipotunukiwa shahada ya kwanza ya habari kutoka chuo kikuu cha Tumaini mjini Iringa. wapili kutoka kulia ni Mrs Mtemahanji yeye alitunukiwa masters ya utawala katika biashara na wa kwanza kushoto ni Mr julius Shayo nae shahada ya kwanza ya habari wakisindikizwa na Junior

Friday, February 27, 2009

usanifu


moja ya madaraja unayokutana nayo unapokwenda dar es saalam

iringa


Saturday, February 7, 2009

NGULI WA NDONDI

JOE CALZAGHE BAADA YA KUPIGANA KWA MUDA MREFU HATIYAYE AMEAMUA KUSTAAFU MCHEZO WA NGUMI

Friday, February 6, 2009

RAIS WA AFRIKA KUSINI


Rais wa AFRICA KUSINI Kgalema Motlanthe, akiwa na spika wa bunge la AFRIKA KUSINI Gwen Mahlangu-Nkabinde, wakiimba wimbo wa taifa kabla hajahutubia bunge na wananchi leo ijumaa

Saturday, January 24, 2009

legal education in tanzania

baadhi ya wanafunzi wa sheria chuo cha tumaini wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wao katika moja ya majengo ya chuo

TUMAINI UNIVERSITY

Mara baada ya kutembelea chuo cha tumaini kwani niliondoka chuoni hapo mwezi wa nane mwaka 2008 mzalendo Thomas Ludovick akanipatia picha hii ili wazalendo wengine waione

Sunday, January 11, 2009

miaka 45 ya mapinduzi ya zanzibar







Leo ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo Watanzania wote wanaungana katika kumbukumbu ya uhuru wa visiwa vya Unguja na Pemba kutoka kwa utawala wa Sultan wa Oman mwaka 1964.
Sherehe za Mapinduzi mwaka huu zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba ambako Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume anatarajia kuongoza sherehe hizo.
Viongozi mbalimbali wa Zanzibar na Muungano wanatarajiwa kuhudhuria na kutoa hotuba za kuenzi mapinduzi hayo ambayo yaliongozwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amaan Karume. Kama ilivyo ada, mbali ya hotuba mbalimbali, sherehe hizo zitapambwa na burudani mbalimbali zikiwamo ngoma za utamaduni kutoka Visiwani na Bara.
Rais Karume pia anatarajiwa kutangaza msamaha kwa wafungwa kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Zanzibar kifungu cha 59. Katika sherehe za mwaka jana, wafungwa 25 walisamehewa. Baada ya Mapinduzi hayo ya Januari 12, 1964, Aprili 26, mwaka huo, Zanzibar iliungana na Tanganyika na kuzaa Taifa moja la Tanzania ambalo Rais wa wake wa kwanza alikuwa Julius Nyerere

Tuesday, December 23, 2008

Ujumbe wa Christmas na mwaka mpya


Every man should be born again on the first day of January. Start with a fresh page. Take up one hole more in the buckle if necessary, or let down one, according to circumstances; but on the first of January let every man gird himself once more, with his face to the front, and take no interest in the things that were and are past.

Saturday, September 13, 2008

DUBAI

Moja ya viwanja vilivyo katika madhari nzuri duniani viko Dubai

Tuesday, September 2, 2008

IBADA

Kanisa hili lilijengwa na wajerumani katika harakati zao za kueneza neno la mungu Tanganyika(Tanzania)pia lina umri mkubwa sana na bado ni imara

Injili






Moja ya kibanda ambacho kilijengwa na wakoloni wa kijerumani katika harakati zao za kueneza injili Tanganyika.Kibanda hiki kiko wilayani Njombe inasadikika kina karne moja na ushehe kwa mujibu ya wanjeji wa Lupembe ambako ndiko kiko,lakini bado kiko imara.Hiyo inayoonekana ni mfano wa biblia takatifu.Asante mzalendo Gosberti wa Njombe kwa picha na maelezo)